EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Monday, May 5, 2014

RULEA SANGA AMUOMBEA EDSON MWASABWITE KWA AJALI ALIYOPATA JUMAMOSI AKIELEKEA DODOMA

Kabla ya yote nimshukuru Mungu kwa kumuokoa mwimbaji huyu maarufu sana nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Mungu tunasema asante kwa kumuokoa na mauti Edson Mwasabwite. Mungu wewe wajua alikotoka, alipo na anakokwenda kwa kazi yako. Tunakemea roho ya mauti kwa ndugu yetu Edson Mwasabwite. Mungu zidi kumlinda mwanao ili azidi kufanya kazi yako. Pale alippopoteza mzidishie. Nimeomba na kushukuru. Amina.

Wako katika Bwana
Rulea Sanga

UFAFANUZI WA AJALI HII
Edson Mwasabwite alipata ajali siku ya Jumamosi mkoani Morogoro katika kijiji cha Dumila iliyosababishwa na mwendasha bodaboda ambaye alikuwa amebeba abiria. Mwendesha bodaboda alikatiza barabarani ndipo walipokutana na Edson.

 Mpaka muda huu mwenye bodaboda na abiria wake wako hospitalini wakiwa hoi sana na gari la Edson liko kituo cha polisi. Akiongea na Rumafrica siku ya leo Edson amesema yuko katika harakati za kwenda kuchukua gari lake na kulileta Dar, na alimshukuru sana Mungu kwa kumuokoa

UNAWEZA WASILIANA NAYE KWA SIMU +255 717 703 415

No comments:

Post a Comment