EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Saturday, May 3, 2014

BLOGA RULEA SANGA ALIA JUU YA MABLOGA WA KIKRISTO

Inasikitisha na haipendezi kabisa kuona watu wa Mungu tunapitwa na watu wa kidunia kwa kuwa serious na mambo yetu. Ni aibu kubwa sana hii na inapaswa kukemewa na Mungu atusaidie tusiabike daima.


Bloga Rulea (kulia) na Mzee Majuto

Mabloga wengi hasa hawa waliokoka wamekuwa wavivu sana ku-upadate blog zao, utaoona blogu ya mpendwa ina miaka na zingine miezi na zingine siku sita hazijawekewa habari mpya. Ninaamini kuna habari nyingi sana zinnaendelea hapa dunia ambazo ni za kumsifu Mungu wetu au kumkashifu Mungu wetu, tunapaswa kama mabloga kuwajuza watu wa Mungu kitu gani kinaendelea.

Inashangaza sana kuona mwimbaji wa nyimbo za injili amefungua blogu yake na anashindwa kuweka habari zake hata za huduma yake. Hatujui huyu mwimbaji kwa mwaka huu ana ratiba gani au kafanya kazi ngapi za kumtukuza Mungu. Kumbuka hawa waimbaji ni kioo cha jamii, na jamii inatakiwa kufuata kile wanachokifanya kwani ni watumishi wa Mungu.

Hii kwa kweli haijakaa vizuri kabisa kwa watu wa Mungu. Tenga muda wako wa kufanya kazi ya Mungu kwa njia ya mitandao. Kuna watu wengi watabarikiwa na wengine kubadilisha maisha yao kwa kupitia wewe mwimbaji au mtumishi wa Mungu. Tunatambua ni ngumu sana kuwafikia watu huko walioko lakini kwa njia ya mitandao utawafikia..

Haya ni yangu na Mungu wangu aguse mioyo yenu juu ya hili

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
+255 715 851523

No comments:

Post a Comment