EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Saturday, September 12, 2015

ASKOFU MH. DK. GERTRUDE RWAKATARE AMUUNGA MKONO MGOMBEA UDIWANI KATA YA KAWE Mh. MUTTA ROBERT RWAKATARE SIKU YA JUMAMOSI


Mgombe Udiwani Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam, Mh. Mutta Robert Rwakatare siku ya leo Jumamosi 12.09.2015 katika viwanja vya Tanganyika Pikers Dar es Salaam aliweza kufungua rasmi kampeni za ugombea Udiwani kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi kata ya Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam


Kutoka kulia ni Mh. Askofu Dk. Gertrude Rwakatare akiwa na mgombea udiwani Kata ya Kawe Bw. Mutta Robert Rwakatare akiwa amemsika mke wake wakielekea katika viwanja vya Tanganyika Pikers Kawe

Katika kampeni hizi kulikuwa na viongozi mbalimbali kutoka kata mbalimbali waliokuja kumuunga mkono Mh. Mutta Robert Rwakatare. Na hii inatokana na ushirikiano wake mzuri na viongozi walioko madarakani akiwa kama Raoisi wa Mchezo wa ngumi Tanzania.

Mgombe Ubunge Kappi Warioba aliweza kufika katika ufunguzi huu wa kampeni akiwa na Mh. Dk. Gertrude Rwakatare ambaye ni mama mzani wa Mutta Robert Rwakatare. Waheshimiwa hawa waliwaomba wananchi kumchangua Mh. Mutta Gertrude Rwakatare kutokana na utendaji wake mzuri katika ujenzi wa Taifa.

Watu wengi waliweza kujitokeza kumuunga mkono Mh. Mutta R. Rwakatare, na hii ni kutokana na kupendwa na wakazi wa Kata ya Kawe.

Mh. Mutta Gertrude Rwakatare aliweza kuomba wakazi wa Kawe kumpigia kura ili akiingia madarakani aweza kuondooa kero za wakazi wa Kawe kama vile Uhaba wa maji, kulikarabati daraja la Kawe, kuboresha elimu, kuinua michezo na burudani kwa wasanii wa muziki nchini, kuikarabati barabara za Kawe, kutetea haki za hati miliki na mengine mengi

Unaweza kutembelea
www.rumaafrica.blogspot.com kujua mengi kuhusu harakati za Udiwani Kata ya Kawe


Askofu Dk. Gertrude Rwakatare

 Mgombea Ubunge Mh. Kippi Warioba aliyevalia shati la yello akielekea jukwaani
 Mzee Makasii akiimba

BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KUONA MATUKIO YOTE YA KAMPENI

Sunday, August 30, 2015

MCH. NOAH LUKUMAYI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B AHUBIRI JUU YA "UMECHAGULIWA KUWA MSHINDI"

Ibada hii ilifanyika siku ya Jumapili 30/08/2015 katika kanisa hili takatifu ambapo mtumishi wa Mungu Mch. Noah  Lukumayi aliweza kuhubiri Neno la Mungu juu ya kibali cha wewe kuchaguliwa kuwa shujaa. Picha hizi zinaonyesha kipindi cha waumini wa kanisa hili wakimsikiliza sauti ya Mungu kupitia mtumishi wake Mch. Noah Lukumayi, na hivi ndivyo ilivyokuwa:


Mchungaji Msaidizi wa kanisa hili Mch. Noah Lukumayi

Nakusalimu kwa Jina la Yesu Kristo. Leo hii tutazungumzia juu ya KUCHAGULIWA KUWA SHUJAA. Mashujaa ni watu wanaomtumaini Bwana na mara nyingi huogopwa na watu, mashujaa hawanung’uniki kwasababu wanafanya makubwa, mashujaa mara nyingi hawaogopi chochote bali wanamuangalia Mungu.


Unaweza kushangaa mbona mambo yako yanabadilika, mambo yako yanaanza kuwa mazuri, hapo tambua ya kuwa kuna malaika wamekuzunguka. Kila mtu anayesali katika kanisa hili la Mlima wa Moto atambue ya kuwa amechagua mahali sahihi na hautashindwa kwa jambo lolote.
Kuna watu watatamani kukusukuma lakini hautaanguka kwani wewe ni shujaa wa BWANA. Mashujaa mara nyingi wamekuwa hawaheshimiki kwasababu wana vita vya kipekee. Kuna maadui wengi sana wanawazunguka mashujaa ili wawaangamize lakini wanashindwa.
 
Niongee na wewe ambaye hujazaa, Mungu yupo pamoja na wewe na atakushindia. Ninaona Yehova akikushindia na kukutetea. Mapito unayopitia sasa yanakwenda kutoweka kwa Jina la Yesu.
Hata kama unapitia magumuzii kumwamini Mungu wako kwani yupo palepale na hajakuacha katika mapito yako. Kila jaribu lina mlango wake wa kutokea, basi amini linakwenda kutokea.

Kuna watu wanakuona huna kitulakini BWANA anakuona wa thamani. Wengine wameweza hata kukudharau na kukutamkia maneno magumu kuharibu maisha lako, lakini nataka kukueleza kuwa BWANA yupo pamoja nawe, zidi kunyeyekea na kumuomba. Unaweza ukaonekana huna thamani lakini BWANA atakuchagua na kuleta mabadiliko mkwa kupitia kwako.
 
Kuna watu watakukatisha tama na kukuvunja moyo, wengine watatamani udondoke lakini wewe simama na BWANA na usitishike wala kuogopa kwani wewe ni shujaa. Kwa kila jambo unalofanya usitegemee akili zako wala usiwategemee wanadamu kwani  yupo Yehova atakayekusaidia.
 
Ukiwa na BWANA, watu watafunga mlango wa mafanikio, lakini utaona mlango huo huo unafunguka. Unachotakiwa kufanyaq ni kuwa mtu wa toba, maombi na shukrani.

Watasema mengi lakini Bwana atakuinua zaidi ya hapo