EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Monday, April 21, 2014

EDSON MWASABWITE AUNGANA NA WAIMBAJI KUTO AFRIKA KUSINI (KEKE) NA KUTOKA ZAMBIA (SEKELETi) KATIKA TAMASHA LA PASAKA 2014 - DAR- UWANJA WA TAIFA


Edson Mwasabwite

Ni mwendo wa mfululizo, wimbo hadi wimbo. Prophet Keke punde baada ya kupanda jukwaani

Son of Tanzania, Ephraim Sekeleti

Babu na nani? Senior bachelor? mi sijui, ila hawa ni Philemon Rupia na Anthon Joseph wa WAPO Radio FM.

Baadhi ya kinadada wa GWT... glory glory..



'vocalists' wa Keke



Kekeletso




Kila mtu kwa raha zake

Baadhi ya umati uwanjani hapo

mtu na 'wajomba'zake

Moja kwa moja kutoka London nchini Uingereza,

Rose muhando, akiwatahadharisha watu kwa kibao chake kipya cha 'fesibuku'.

Kwani ni jambo lipi hilo yeye asiloliweza? Sarah K anauliza..

Tuesday, April 15, 2014

HATIMAYE EDSON MWASABWITE KUACHIA ALBAMU YA PILI YA MUNGU TU AMENIHURUMIA ASILIMIA 100.

Edson Mwasabwite katika ofisi za Rumafrica
Baada ya albamu ya kwanza kufanya vizuri, Edson Mwasabwite ameachia albamu yake ya pili ya Mungu tu amenihurumia asilimia 100. Akiongea na Rumafrica siku ya jana, alimshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha kutunga nyimbo na hatimaye kumaliza ablamu yake ya pili ambayo amesema itakuwa baraka kwa walio wengi. Pia aliwaomba watu wa Mungu waipokee hii albamu kwa maana kuna ujumbe malidadi sana katika maisha yao. Edson Mwasabwite hakuishia hapo, aliongeza kwa kusema  watu wasinunue albamu ambazo ni feki kwani hawatapata ubora na muziki mzuri na pia watakuwa wanawaonyonga waimbaji kimapato.

Rumafrica iko mbioni kufanya mahojiano na mwimbaji huyu ambaye amepata mafanikio makubwa kwa kumuimbia Mungu, na watu wengi wamebarikiwa sana na huduma yake na imefika kipindi watu wanapiga nyimbo zake hata  katika bara kutoka na jumbe zenye mguso wa ajabu.

MTU NA KAKA YAKE, GRACE NA JOSHU KUACHIA ALBAMU YAO YA KWANZA YA MY SAVIOUR GOD

Baada ya kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali, Grace na Joshu wameamua sasa kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu. Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya albamu yao hii ya kwanza.

Grace Christian Rwegasha

Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili  ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo za Kiingereza.

Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma yao  ya uimbaji.

Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.

Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao kuwashirikisha

Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu mbalimbali.

Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya kazi  ya Bwana.

Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya utakaposikia mahojiano yetu.

Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080

MUNGU AKUBARIKI