Edson Mwasabwite katika ofisi za Rumafrica
Baada ya albamu ya kwanza kufanya vizuri, Edson Mwasabwite ameachia albamu yake ya pili ya Mungu tu amenihurumia asilimia 100.
Akiongea na Rumafrica siku ya jana, alimshukuru sana Mungu kwa
kumuwezesha kutunga nyimbo na hatimaye kumaliza ablamu yake ya pili
ambayo amesema itakuwa baraka kwa walio wengi. Pia aliwaomba watu wa
Mungu waipokee hii albamu kwa maana kuna ujumbe malidadi sana katika
maisha yao. Edson Mwasabwite hakuishia hapo, aliongeza kwa kusema watu
wasinunue albamu ambazo ni feki kwani hawatapata ubora na muziki mzuri
na pia watakuwa wanawaonyonga waimbaji kimapato.
Rumafrica iko mbioni kufanya mahojiano na mwimbaji huyu ambaye amepata mafanikio makubwa kwa kumuimbia Mungu, na watu wengi wamebarikiwa sana na huduma yake na imefika kipindi watu wanapiga nyimbo zake hata katika bara kutoka na jumbe zenye mguso wa ajabu.

No comments:
Post a Comment