EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Saturday, May 10, 2014

HABARI INATOKA KWA SAMSASALI: MWANAMUZIKI WA INJILI EDSON MWASABWITE AKANUSHA KUOMBA SUPPORT YA KUTENGENEZA GARI LAKE


Mwanamuziki Wa Injili Tanzania Edson Mwasabwite anayetamba na wimbo wake wa Kwa Neema amefunguka na kusema kuwa matangazo yanayosambazwa kwa ajili ya Kusupport kutengeneza gari lake upya amekanusha kuwa yeye ndiye aliyeomba suala lifanyike.

Blog hii imekutana na Mwanamuziki huyo mtaani na kutaka kufahamu chanzo cha ajali hiyo na anasemaje juu ya michango inayokusanywa kwa wadau wa nyimbo za injili ili kuweza ku-support utengenezaji wa gari hilo. Edson Mwasabwite anasema "sijashirikishwa kuhusu ukusanyaji wa fedha hizo, na kama zitanifikia basi nitapeleka kwenye kituo cha Watoto Yatima kwa Sababu gari langu lina Bima Kubwa"



Mwanamuziki huyo ambaye alipata ajili hiyo ya gari alilokuwa akiendesha yeye mwenyewe kutokea Dodoma kwenda Morogoro Kwenye huduma. Akiongea na Blog Ya hii na James Temu ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa boda boda aliyeingia ghafla katika barabara kuu akitokea kwenye mchepuko.

Edson anasema anamshukuru Mungu kwa kumponya na ajali hiyo na kwa sasa gari iko kwa Wachina kwa ajili ya Matengenezo.



MSIKILIZE

No comments:

Post a Comment