EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Saturday, May 3, 2014

MARGRETH SEMBUCHE KUACHIA ALBAMU YAKE YA “MSAFARA WA MAMBA”


Margreth Sembuche kwa wasio mjua ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Mungu amekuwa akimtumia sana kwa karama yake ya uimbaji kwa muda mrefu sana. Huduma yake imekuwa na mguso mkubwa kwa waliobahatika kusikia nyimbo zake kama sehemu mbalimbali. Kwa sasa ametoa albamu yake ya kwanza inayoitwa MSAFARI WA MAMBA na katika albamu hii kuna nyimbo 8 ambazo ni

1. Msafara wa mamba 2. Nyakati 3. Utandawazi  4. Ngome 5. Yatima 6. Heka Heka 7. Jibu unalo mwenyewe 8. Jina la Yesu

Albamu yake iko katika mfumo wa video (DVD) na Audio. Huu ni wakati wako kusikiliza nyimbo mpya na kuona jinsi Mungu anavyowatumia watu hapa dunia katika kujitwalia utukufu.

Rumafrica ipo katika harakati za kumtafuta Margreth Sembuche kwa mahojiano. Endelea kutembelea blogu yetu.

Unaweza kuwasiliana naye kwa simu hii +255 717 163 146

No comments:

Post a Comment