Kuna mambo mengi utaenda kujua kupitia mwimbaji huyu wa nyimbo za
Injili Tanzania, Grace Rwegasha. Mwimbaji huyu haimbi peke yake bali
anashirikiana na mdogo wake Joshua (Joshu). Ngoja tusome haya mahojiano
yaliyofanyika katika ofisi ya Rumafrica hapa Afrikasana Dar es Salaam
Tanzania
Rumafrica: karibu sana katika ofisi zetu za Rumafrica, tunaomba ujitambulishe.
Grace Rwegasha:
Nashukuru sana ndugu mtangazaji kwa kunikaribisha katika ofisi yako
ili kuweza kujieleza, kwa jina naitwa GRACE RWEGASHA, katika huduma hii
nimeimba na mdogo wangu anaitwa JOSHUA RWEGASHA ambaye sipo naye hapa
yupo Mwanza anamalizia masomo yake ya University ST. AGAST.
Grace Christian Rwegasha
Rumafrica: Ni aina gani ya music mnapiga?
Grace
Rwegasha: Sisi tunaimba nyimbo za Injili, mdogo wangu JOSHUA anakipaji
cha uimbaji na anapenda kuimba kwa lugha ya kingereza. Toka akiwa mtoto
alikuwa anapenda kuimba, anatunga nyimbo na baada ya kuwa mkubwa aliweza
kuniambia dada twende tukarekodi, kwa hiyo ni huu mwezi wa nne ndio
tumerekodi albamu yetu ya kwanza.
Rumafrica: Albamu yenu inaitwaje?
Bloga Rulea Sanga wa Rumafrica
Grace Rwegasha: Albamu yetu inaitwa MY SAVIOUR GOD
.
Rumafrica: ni lini ulianza hudua hii ya uimbaji wa nyimbo za Injili?
Grace Rwegasha:
kwa kweli kuimba kupo kwenye damu yangu, wakati mwingi napenda kusifu
na kuabudu, kwa hiyo kipaji cha kuimba ni kitu ambacho kilikuwa moyoni
mwangu, lakini nilikuwa sijajipanga kwenda kujitokeza kwa watu kuimba,
lakini mdogo wangu ndiye aliyenivuta akasema dada twende tukarekodi.
Sijawahi kuimba kwenye kwaya yoyote lakini mimi mwenyewe tu nilikuwa
napenda kuimba.
Rumafrica: Ni siku gani ambayo mliingia rasmi studio kwenda kurekodi?
Grace Rwegasha: Siku
ambayo tuliingia studio rasmi kwenda kurekodi ilikuwa ni mwezi wa
kwanza kwa huu 2014. Mdogo wangu JOSHUA alisema kwamba kuimba kumetawala
sehemu kubwa ya maisha yake kwa sababu muda mwingi anautumia kwenye
kutunga nyimbo, nyimbo zake zinafika zaidi ya elfu tano, kwa hiyon
twende tukarekodi.
Rumafrica: kwa nini albamu yenu inaitwa MY SAVIOUR GOD?
Grace Rwegasha:
Albamu yetu tulipenda kuiitwa MY SAVIOUR GOD kwa sababu pia kuna wimbo
unaitwa My Seviour God, nakumbuka siku ya huo wimbo Joshua aliamka
alfajiri sana akaniambia Grace mimi nimepata wimbo, mimi nilijua kwamba
wimbo huo ameshushiwa kutoka juu mbinguni kwa hiyo wimbo huo tukaupa
jina la MY SAVIOUR GOD, Mungu anakwenda kutuinua kupitia wimbo huu.
Rumafrica: Albamu yenu inanyimbo ngapi?
Grace Rwegasha: Albamu
yetu kwa sasa ina nyimbo 12, tuliamua tufanye nyimbo 12 kwa sababu
tulipofikia kutaka kutoa Albamu watu walituambia kwamba nyimbo zetu
hazitanunuliwa kwa sababu watu wengi huwa hawapendi nyimbo za kingereza.
Lakini sisi tukasema sasa tufanyeje kwa sababu Mungu anatushushia
nyimbo za kingereza, tukaona kwamba tukiziacha itakuwa ni kama mtu
umewasha taa alafu ukaiweka chini ya uvungu wa kitanda. Ndipo tulienda
studio kurekodi lakini tukaamua tuchanganye kwa hiyo tumefanya 9
kiswahili na 6 kingereza.
Rumafrica: Tungependa kujua majina ya nyimbo zilizopo katika Albamu yenu?
Grace Rwegasha:
Nyimbo zilizopo kwenye albamu yetu majina yake ni MTENDA MIUJIZA,
GEUKA, YUHAI, MJI WA MUANGAZA. Na za kingereza kuna MY SAVIOUR GOD, ALL
MY HAND, PARADISE.
Rumafrica: ni nyimbo gani unaipenda sana katika albamu yenu?
Grace Rwegasha:
Wimbo ambao ninaupenda sana ni MY SAVIOUR GOD, ni wimbo ambao unanigusa
sana katika moyo wangu, pia ninaupenda wimbo wa TENDA MIUJIZA, kwa
kweli Bwana anatenda miujiza mpana nimefikia kuimba hiyo ni miujiza.
Rumafrica: Style gani ya uimbaji mnatumia?
Grace Rwegasha:
style zetu tumechanganya, nyimbo nyingine tunaweza tukacheza Quito,
nyingine tunaweza tukacheza Charanga, kwa hiyo tumechanganya changanya
hatujacheza katika style moja. Kwa kweli tumependa kufanya hivyo kwa
sababu ili tuweze kufafuraisha watu zaidi, kwa mfano utakuta kuna yimbo
ya harusi, nyimbo ya kuabudu.
Rumafrica: Tungependa kusikia akapela ya wimbo mmoja.
Grace Rwegasha:
Naomba niimbe wimbo wa MTENDA MIUJIZA:…… Yupo mtenda miuujizaa, yupoo
yupoo, yupo na atakuwepo, yupooo yupooo, Yesu wa kabila la Yudaaa,
mwana wa Mungu aliye haii, Yesu wa kabila ya Yuda mwana wa Mungu aliye
haiii.
Rumafrica: ni studio gani mmerekodi nyimbo zenu?
Grace Rwegasha:
Nyimbo zetu tumerekodia kwa produce anaitwa RICK, kwa kweli huyu
produce amekuwa mtu mzuri sana kwangu, alitupokea vizuri tulikuwa
tunakatishwa sana tamaa kwamba nyimbo za kingereza hazitanunuliwa lakini
produce Rick akasema hapana Watanzania wanapenda sana nyimbo za
kingereza na nyimbo zenu ni nzuri mtafika nazo mbali. Na pia alitushauri
tutunge na nyimbo za Kiswahili japokuwa zilikuwa chini ya kiwango, basi
tuliweza kutunga mpaka zikafikia nyimbo 9.
Rumafrica: Watu wanasema nyimbo za kingereza hazina upako kwa Watanzania, unasemaje?
Grace Rwegasha:
mimi ninaujasiri mkubwa sana kwamba Watanzania wanapenda nyimbo za
kingereza, labda sisi Watanzania hatujafikia kiwango cha kuweza kutunga
nyimbo za kingereza tunajaribu jaribu, lakini kwa mtazamo wangu
Watanzania wanapenda nyimbo za kingereza.
Rumafrica: Changamoto gani mnazipata katika huduma yenu ya uimbaji?
Grace Rwegasha: Changamoto
tunazozipata ni nyingi hasa kwa marafiki ambao nilikuwa nao kabla
sijaenda studio, ukiwaomba ushauri wanakwambia wewe sauti yako sio nzuri
usiende, wengine wananiambia wewe nenda katafute shamba ulime, wengine
wananiambia nenda kafuge kuku kwani hautaweza kuimba. kwa hiyo
ukisikiliza watu unaweza usifikie lile lengo ambalo Mungu anataka
ulifanye, kwa hiyo hizo ndo changamoto na kama nilivyotangulia mwanzo
kusema walikuwa wanatukatisha tamaa kuimba nyimbo za kingereza,
nilichojifunza ni kwamba sikiliza Roho wa Mungu anakwabia fanya nini.
Pia kuna studio moja ambayo tulienda, kwa kweli produce alitutesa sana,
tulimpatia fedha tukarekodi nyimbo, lakini fedha nyimbo mpaka leo
hatujaviona, na dhani ni miaka 2 sasa imepita, lakini sisi tumemsamehe
ila tu hizo nyimbo zetu asije akazitoa popote. Kwa hiyo ni changamoto
mbaya sana ambayo tuliipitia kabla hatujakutana na huyu Produce Rick.
Rumafrica: Je mlichukuwa hatua yoyote kwa huyu aliyewatapeli fedha zenu za studio?
Grace
Rwegasha: kwa kweli tuliwaza sana kuhusu hilo, lakini tukaona kwamba
kwa sababu sisi tulitaka kumtumikia Mungu, na hichi kitu ni cha
kumtumikia Mungu, huwenda sio yeye aliamua kufanya hivyo bali ni
shetani, kwa hivyo sisi tukiamua kumchukulia hatua tutakuwa tukipigana
na mtu badala ya kupigana na shetani, na ili tuweze kumshinda shetani
tuliamua kumsamehe.
Rumafrica: Jamii imefaidika nini na huduma yenu?
Grace Rwegasha:
Huduma yetu ndo tumeanza, tunaimani Mungu atatubariki na ipo siku
atatupa kitu mkononi cha kuweza kuisaidia jamii, kwa sasa tumetoa nyimbo
ili watu wapokee kwaajili ya Roho zao.
Rumafrica: Kwa nini waimbaji wanatanguliza pesa na huduma baadaye?
Grace Rwegasha:
ni kweli, ila kwa sasa hivi inabidi waimbaji tubadilike kwa sababu
tumejiachia sana, tumesahau kuwa sisi ni watumishi wa Mungu tumeenda
kibiashara zaidi. Kwa mfano biblia inasema mmepata bure toweni bure,
ndio najua mwimbaji anategemea pale ndio atakula na kufanya mambo yake
mengine lakini Bwana Yesu anasema tumtegemee yeye kwa kila jambo na
yeye atafanya. Kwa hiyo inabidi mtu anapoitwa asiweke kiwango cha fedha
ndio akatoe huduma, kama tumeamua kumtumikia Mungu basi tumtumikie Mungu
kweli nayeye atatubariki.
Rumafrica: Unasemaje juu ya hawa wanaotegemea uimbaji?
Grace Rwegasha:
Mimi ninafikiri hilo kwa sababu na Wachungaji nao wanajua ni watoto
wadogo ambao Bwana anawainua na wanategemea hivyo watawapa zawadi.
Lakini mimi kitu ambacho naweza kupinga ni pale ambapo mchungaji
amekuita uende kuimba akakwambia nitakupa kiasi kadha cha fedha mwambie
mchungaji asante mimi nakuja, lakini kitendo cha kukataa na kusema
hapana bila kufikisha milioni 5 mimi siji, kwa kweli hapo tunakuwa
tunamkosea Mungu.
Rumafrica: Kwa nini ndoa za waimbaji hazidumu?
Grace Rwegasha: Kwa
kweli hilo swali ni gumu sana kulijibu, ila ngoja niseme mimi kwa
mtazamo wangu, mtu yeyote Yule ambaye ni mtumishi shetani utafuta njia
nyingi sana za kuweza kumwangusha, shetani akikukosa kwenye pombe lazima
atatafuta pale ambao mpo waili kwenye ndoa, au kwenye udhaifu ni wapi,
kwa hiyo shetani utafuta mbinu na kila namna ili tu avuruge. Kwa mfano
labda mama umeachwa nyumbani badala ya kuamini kwamba baba ameenda
kuhubiri, au mume wangu ni mwimbaji na ameenda kuimba kweli wewe unaanza
kuwaza tofauti kwa sababu pia shetani uingia kwa njia ya mawazo, kwa
hiyo unavyowaza vile na shetani naye hupata nafasi ya kuweza kuvuruga
ndoa yako. Kwa hiyo inabidi pia tuwe waombaji ili tuweze kumshinda
shetani.
Rumafrica: Ni kwa nini mchungaji anatenda maovu mitaani lakini bado anakuwa na upako wa miujiza madhabahuni?
Grace Rwegasha:
Mimi ninachopenda kusema ni kwamba jina Yesu lenyewe linajitegemea, ila
Mungu wetu ni Mungu mwenye huruma na rehema nyingi, kwa hiyo ukimuona
mchungaji ameenda katika njia ambazo sizo ujue bado yupo katika mkono wa
Mungu wenye rehema. Kwa sababu Mungu hapendi mtu Yule apotee aende
jehanamu
.
Rumafrica: Unasemaje juu ya watumishi wanaokamatwa na maovu na baada ya kukamatwa wanakimbilia nchi nyingine na kuanzisha huduma huko?
Grace Rwegasha:
Mimi ninachopenda kusema ni kwamba hautakiwi kukimbia, bali unapaswa
kutubu mbele za Mungu wako na mbele za watu, na uwe umedhamiria kuomba
toba ya kweli maana Mungu anaangalia ndani ya moyo. Unaweza ukasema
mbele za watu mnisamehe kumbe wewe hujafanya toba ya kweli na Mungu
wako, kwa hiyo ukifanya toba ya kweli na Mungu atauondoa ule uovu, kwa
hiyo utakuja kushangaa kwamba watu hawata libeba lile jambo kwa huzito
kama ambavyo ungefikiria kukimbia. Lakini endapo utakimbia huko
unapoenda nako Mungu anakuangalia unafanya sawa au sio sawa, na mpaka
ufika hiyo nchi nyingine ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu
ungeweza ukafia njiani, kwa hiyo kuna haja ya kutubu na kumrudia Mungu.
Rumafrica: Unasemaje juu ya watu wanaotangatanga mara wamwimbie Mungu na mara waimbe nyimbo za kidunia na sio za Mungu?
Grace Rwegasha:
Ukisoma katika kitabu cha Waebrania 10:26…, Biblia inasema: Maana kama
tukifanya dhambi kusudi baada ya kupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki
tena dhabibu kwaajili ya dhambi, bali kuna kuitazamia hukumu yenye
kutisha, na ukali wa moto ulioyatayari kuwala wao wapingao, mtu
aliyeidharau sheria ya Musa, hufa pasipo huruma kwa neno la mashahidi
wawili au watatu … Napenda kuwaonya kwa Roho mtakatifu wale ambao
wanapenda kufanya hivyo waache, wamtumikie Mungu katika Roho na kweli,
maana hapa duniani sio petu, utajiri tunaoutafuta hautatufikisha popote,
hata ukijenga majumba utayaacha, tengeneza kwanza kwaajili ya ufalme wa
Mungu. Kwa kweli mimi ninafuraha sana kwa wale wanaotoka katika nyimbo
za kidunia na kumuimbia Mungu, kwa sababu Yesu mwenyewe anasema mimi
ndiye njia ya kweli na uzima, mtu aji kwa baba isipokua kwa mimi yaani
Yesu Kristo. Na yeye Yesu ndiye mlango kwa hiyo sisi kama waimbaji wa
nyimbo za Injili tunamwimbia Kristo na ili watu wengine waje katika huu
mlango.
Rumafrica: Asante sana kwa kuwa na wewe na karibu
sana katika office zetu za Rumafrica, na Mungu akubariki sana katika
karama yako ya uimbaji, na naimani Mungu atakuinua sana utatoka hapo na
utakuwa muhubiri.
Grace Rwegasha: Halleluya, namuomba Mungu anipe hiyo nafasi.
UNAWEZA KUWASILINA NAYE KWA SIMU +255 788 443 346