EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Thursday, March 20, 2014

ISEMAVYO MITANDAO: RUMAFRICA YASEMA - JAMANI KUPENDEZA SIO DHAMBI

Chanzo cha Habari bonyeza hapa: RUMAFRICA

Mungu anavyokuinua lazima uonyeshe kuwa kweli Mungu kaniinua. Sio Mungu anakuinua na wewe unaonekana kama vile hujainuliwa, unaamuabisha Mungu wako. Hebu fikiria mtu anakupa zawadi ya nguo na wewe huvai ile nguo, huyo mtu atajisikiaje..?

Tusimwaibishe Mungu wetu. Angalia watu wa mataifa wanavyopendeza jamani. Ni kweli tunatafuta kwenda mbinguni lakini yatupasa kuonyesha mataifa kuwa Mungu wetu anatupenda na anatubariki ili watu wajue kuwa kwa Mungu kuna faida. Tusijionyeshe choka mbaya, hii haipendezi kabisa machoni pa watu na machoni pa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kuwa smart kiroho na kimwili. Furahia maisha yako hapa duniani  na huko tuendako mbinguni tiukafurahi na Bwana. Acha kujinyima na kuishio maisha kama mtu aliyechukiwa na Mungu. Mungu wetu anapenda kuona watu wake wanabarikiwa na kufuraha hapa duniani. Pia Mungu wetu anapenda kuona unakuwa msafi KIROHO na mtu wa kumpenda YEYE.

Edson Mwasambwite tunakupa Big Up kwa kutokelezea na Mungu akubariki na akupe maisha marefu duniani.

Wenu katika Bwana

Rulea Sanga

No comments:

Post a Comment