EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Monday, March 17, 2014

ISEMAVYO MITANDAO: MAKALA : EDSON MWASABWITE NI KWA NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU KUWA HAPA NILIPO - 2013

Wednesday, 3 April 2013
Habari inatoka : GOSPEL KITAA




"Hapa nilipo mimii ni kwaneema ya Mungu, vile nilivyo mimi ni kwa neema ya Mungu, nimetoka mbali toka mbali toka mbalii nimetoka mbaliii...... Ni kwaneema tu na rehemaa, ni kwa neema tu na rehemaa" Hayo ni baadhi ya maneno katika wimbo Ni kwa neema na Rehema uliomtambulisha kijana Edson Zako Mwasabwite ambaye kwasasa ana album moja yenye jumla ya nyimbo nane ikibebwa na wimbo huo, huku akiwa mbioni kukamilisha album yake ya pili. Edson ni mzaliwa wa mkoani Mbeya ambaye alitambua kipaji chake cha uimbaji wakati akiwa shule ya jumapili au Sunday school huko Rungwe mkoani Mbeya

Edson aliachwa yatima kwakuondokewa na wazazi wake ambapo wimbo wa Ni kwa neema na Rehema amesema unaelezea jinsi neema na rehema ya Mungu ilivyomtetea na kumfikisha hapa alipo maana asingekuwa Mungu labda ingebaki historia tu kutokana na masiha magumu aliyoishi. Amesema yeye ni kijana aliyeokoka anampenda Mungu, anaabudu katika kanisa la Kilutheri Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Album yake hii yenye nyimbo nzuri zakutia faraja, kusifu na kuabudu ilianza kupendwa mikoani hususani mikoa ya Iringa na Mbeya ambako watu wengi hupenda kusikiliza wimbo Ni kwa neema, GK ilikutana kwa mara ya kwanza na Edson miaka miwili iliyopita alipofika studio za WAPO Radio Fm kurasini jijini Dar es salaam kuleta album yake hiyo ambapo ndani ya wiki moja tangu kuanza kupigwa alipata mwaliko wa kwenda kuimba kwenye kituo cha maombi na maombezi BCIC Mbezi beach kilicho chini ya WAPO mission International, Edson alifurahi sana kupata nafasi hiyo.

Akiwa tayari ametambulishwa vyema na album hiyo Edson anasema ana kila sababu ya kumshukuru Mungu alipofikia kwakuwa amekutana na changamoto nyingi sana wakati anaanza kuimba kama mwimbaji binafsi, changamoto hizo ni pamoja na ushauri mbaya kutoka kwa watu ilimradi ushindwe kwenye huduma, suala la fedha ambalo hukwamisha mambo mengi hasa unapokuwa huna kipato chochote na unataka kurekodi album yako, lakini pia Edson amesema kuna tatizo la kutokuwepo kwa ushirikiano baina ya waimbaji wakongwe waliopo kwenye muziki kwa muda mrefu na wale wachanga hali ambayo inasababisha kutopata njia sahihi ya mwelekeo hasa linapokuja suala la wasambazaji ambao kwa mwimbaji mchanga hujui vizuri kinachoendelea kama ilivyokwa wazoefu ila anamshukuru Mungu mambo yanakwenda vizuri kwasasa.

Kilio chake Edson kwa waimbaji wenzake ni kutaka wawe barua inayosomwa vyema na watu wanaowahubiria ili maneno na matendo yawe sawa na kubariki pamoja na kuwavuta watu kwa Yesu zaidi kuimba kwao isiwe hapa duniani pekee bali siku moja wakajiunge na jeshi kubwa la malaika mbinguni kumsifu Mungu zaidi amewataka waimbaji kwa pamoja wasiwe kama vibao kuonyesha njia wakati vyenyewe havifiki kunakotakiwa.

Edson akiwa katika madhabahu ya BCIC Mbezi beach.

No comments:

Post a Comment