Monday, December 16, 2013
Bonyeza hapa kujua chanzo cha habari: SAMSASALI BLOGU
EDSON MWASABWITE: Mwimbaji Injili aliyetoka mbali....Ni Kwa Neema Tu
Asema
alivyo leo ni kwa neema tu ya Mungu
“HAPA nilipo mimii ni kwa neema ya Mungu, vile
nilivyo mimi ni kwa neema ya Mungu, nimetoka mbali-toka mbali toka mbalii
nimetoka mbaliii…… Ni kwa neema tu na rehemaa, ni kwa neema tu na rehemaa.”
Hayo ni baadhi ya maneno katika wimbo wa ‘Ni kwa
Neema na Rehema’ uliomtambulisha vema kijana Edson Mwasabwite, ambaye kwa sasa
ana albamu moja yenye jumla ya nyimbo
nane ikibebwa na wimbo huo, huku akiwa mbioni kukamilisha albamu yake ya pili.
Albamu hiyo yenye nyimbo za kutia faraja, kusifu na
kuabudu ilianza kupendwa mkoani Iringa na Mbeya ambako watu wengi hupenda
kusikiliza wimbo wa ‘Ni kwa Neema na Rehema’.
Akiwa ametambulishwa vema na albamu hiyo, Mwasabwite
anasema ana kila sababu ya kumshukuru Mungu alipofikia kwa kuwa amekutana na
changamoto nyingi sana wakati anaanza kuimba kama mwimbaji binafsi.
Edson aliachwa yatima kwa kuondokewa na wazazi wake
ambapo wimbo wa ‘Ni kwa Neema na Rehema,’ amesema amejaribu kuelezea jinsi
neema na rehema ya Mungu ilivyomtetea na kumfikisha alipo, maana asingekuwa Mungu labda ingebaki
historia tu kutokana na maisha magumu aliyopitia. Amesema yeye ni kijana
aliyeokoka, anampenda Mungu, anaabudu katika Kanisa la Kilutheri Kijitonyama,
jijini Dar es Salaam.
Kilio chake Edson kwa waimbaji wenzake ni kuwasihi
kuwa barua inayosomwa vema na wanaowahubiria ili maneno na matendo yawe sawa na
kubariki pamoja na kuwavuta watu kwa Yesu zaidi kuimba kwao isiwe hapa duniani
pekee bali siku moja wakajiunge na jeshi kubwa la malaika mbinguni.
Edson anawasihi waimbaji wasiwe kama vibao kuishia kuonesha njia wakati vyenyewe haviendi huko kunakotakiwa.
Edson anawasihi waimbaji wasiwe kama vibao kuishia kuonesha njia wakati vyenyewe haviendi huko kunakotakiwa.
Anasema kuwa hafungwi kuabudu katika kanisa lolote
na ikiwa atapokea maono ya kuhama, basi
atafanya hivyo.
Anasema wimbo wake wa ‘Ni kwa Neema na Rehema’,
aliimba kwa sababu hakutarajia kama angefika alipo, kwani ni kwa neema tu,
kwakuwa aliishi maisha magumu baada ya kuachwa yatima.
“Hii ni historia ya maisha yangu. Wokovu wenyewe ni
kwa neema, nikiangalia vijana wengine mimi niko salama zaidi,” anasema.
Mafanikio“Mafanikio yapo, japo kwa mtu mwingine yanaweza
kuonekana kama sifuri, ila mafanikio inategemea na huyo mtu yuko katika nafasi
au ngazi gani. Ingawa ndiyo nimeanza, naona mafanikio, namshukuru Mungu,”
anasema.
ChangamotoEdson anasema changamoto katika uimbaji zipo, hasa
kwa chipukizi, kwani mtu anapoanza
kuimba unakuta hana fedha, mara nyingine inakuwa ni kikwazo ili kuweza kuweka
uimbaji katika viwango vya juu.
Anasema changamoto nyingine ni watu wengine kushauri
vibaya kwa makusudi ili uanguke.
“Hakuna ushirikiano kwa wale walio wazoefu katika
muziki wa Injili, hii imesababisha hata hasara, kwa kuwa unakosa mwongozo kutoka kwa wazoefu.
“Lakini pia kuna changamoto ya utaalamu,
wasikilizaji na jamii kwa ujumla hawajaupa nafasi sana muziki wa injili. Watu
wengi wanauchukulia kama burudani tu, suala la kuelimisha na kusisimua.
“Ila tunashuru Mungu kwamba watu wanatuunga mkono.
Ndiyo maana utakuta nyimbo zinazohit ni zile za kuburudisha zaidi. Kwa Tanzania
Mungu ameupa muziki wa Injili Neema,” anasema.
Anaongeza kuwa, kwa sasa anaishi Dar es Salaam.
Kuhusu suala la kuoa anamuomba Mungu ampe mke mwema, kwani ni heri ukosee
kujenga nyumba au kurekodi wimbo utaurudia lakini si kuoa.
Ushauri“Ujumbe wangu kwa waimbaji wenzangu wa nyimbo za
Injili, wajue kama unahubiri, uwe mfano na wakili, tusiwe kama vibao, lakini
tusiende huko. Yesu alisema itamfaa nini mtu apate vya dunia na kuikosa mbingu.
“Wito wangu kwa watu wote ni wawe tayari kuelimishwa
pia na nyimbo za Injili na si kuburudika tu, wajue tunaishi kwa neema tu, wajue
Mungu ndiye ametupa vyote tulivyo navyo, ambao hawajaokoka wampokee Yesu
Kristo.
Vyote tulivyo navyo bila Kristo ni bure, wajiulize
wataishi wapi baada ya maisha haya.
“Tuwe barua, mtu akituona ajue kweli huyu anamwimbia
Mungu aliye hai. Tujiandae kuimba mbinguni, si kupata sifa hapa duniani na kwa
waimbaji chipukizi, kwa wanaoanza wasikate tamaa, kwani hakuna aliyezaliwa
akiwa na jina, wala vitu, wawe wavumilivu na waaminifu mbele ya Mungu ili
wafanikiwe,” anasema.
Historia
Edson alizaliwa Meta, Mkoa wa Mbeya, Aprili 24, 1983 na kupata elimu ya msingi Mtaba.
Edson alizaliwa Meta, Mkoa wa Mbeya, Aprili 24, 1983 na kupata elimu ya msingi Mtaba.
Anasema kuwa kipaji chake cha uimbaji kilitambuliwa
akiwa Shule ya Jumapili ‘Sunday School’ Rungwe, mkoani Mbeya.
Anasema kuwa katika familia yao wamezaliwa watoto
watatu kwa upande wa mama yake.
Anaeleza kuwa yeye ni mtoto wa nje ya ndoa na
alilelewa na mama yake, ambapo hakumfahamu baba yake hadi alipofika darasa la
nne.
“Nimeishi maisha magumu sana yenye changamoto za
kila aina, yaani unaishi na mama ambaye ni mkulima, maskini na kama unavyojua
maisha ya kijijini wakati mwingine
hakuna kula, kuni zimelowa au kukosa hela ya chakula,” anasema.
Anasema kuwa baada ya kumfahamu baba yake alikaa
naye kwa miaka mitatu na akafariki dunia mwaka 1999 na ndipo matumaini ya
kusoma yakapotea. Anaeleza kuwa miaka michache baadaye mama yake alianza
kuugua.
“Nilimuuguza mama yangu huku nikilea familia,
aliugua kwa muda wa mwaka mmoja na nusu na alifariki dunia mwaka 2005, yaani
hapo ndoto zote zilikufa, ila namshukuru Mungu maana mimi niliokoka mapema,
ilinisaidia kutokujiunga katika makundi ya kihalifu, maana hofu ya Mungu
ilikuwa ndani yangu,” anasema.
Mbio
za umaarufuAnasema kuwa mbio zake za uimbaji zilianza rasmi
mwaka 2007 na kuanza kutafuta michango, lakini hakupata.
“Kuna watu siwezi kuwasahau, walinisaidia sana
katika harakati zangu za uimbaji, yaani mtu kama Angonile, Sifa Mwankili na
Mama Nisa, hawa walikuwa wakinipatia fedha na hata kunikopesha, ila
sikufanikiwa na nikarudi kijijini,” anasema.
Anaeleza kuwa baada ya mwaka huo kutofanikiwa
alirejea tena Dar es Salaam 2010 akiwa
hana mfadhili, anasema kuwa maisha yalikuwa magumu sana japo alifanikiwa
kurekodi albamu hiyo.
“Baada ya kurekodi, nilirudi nayo kijijini na ndipo
niliugua TB, nikatibiwa na kupona, lakini maisha yakawa ya taabu sana, nikawa sina hela, madeni mengi, kazi haipo
sokoni, ninayo ndani,” anasema.Anasema hawezi kumsahau Ephraim Mwansasu, kwani
ndiye aliyemsaidia kumpeleka kwa wasambazaji na albamu hiyo ambayo inapendwa na
wengi.
Usiyoyajua
-Muimbaji huyo hajaoa, hana mtoto.
-Albamu yake ya ‘Ni Kwa Neema na Rehema’ aliirekodi
mwaka 2010.
-Alikuwa akifanya biashara ya kahawa mbichi.
-Kanisa halikumkubali na kipaji chake
-Maisha yake yote hakujua wala kuhisi kama angekuwa
maarufu.
-Ni yatima.
-Wamezaliwa watatu, wa kiume wawili na wa kike
mmoja.
-Alisaidiwa na rafiki zake kuweza kuingia studio.
-Aliokoka mwaka 2001.
-Aliishi akilea familia ya watu saba.
-Wasambazaji ndio wapanga bei ya kazi.
Albamu
Albamu yake ya kwanza ina nyimbo nane ambazo ni ‘Ni
Kwa Neema na Rehema’, ‘Tarajia Mujiza’, ‘Asante Yesu’, ‘Usiwe Mbali Nami’,
‘Bwana Yesu’, ‘Atanifuta Machozi’, ‘Milele Usifiwe’ na ‘Mungu Wetu Anaweza’.
Akizungumzia ujio wa albamu yake mpya, Edson anasema
itakuwa na wimbo ambao utatoka Desemba mwaka huu.
Anasema albamu hiyo itaitwa kwa jina la
‘Amenihurumia asilimia mia’, ikiwa pia na nyimbo kama ‘Nikiwa na umri wa miezi
Nane’, ‘Kweli ni Mimi’, ‘Mkono Wako’, ‘Uwe Nami’, ‘Nitamwimbia Bwana’, ‘Wewe ni
Mshindi’, ‘Mtetezi Wetu yu Hai’, ‘Tumia Vizuri Nafasi’ na ‘Kyala Nnunu’.
Anasema kuwa albamu hiyo ameirekodi Cke Studio ikiwa
na mahadhi mbalimbali kama rhumba, kwaito, zouk na sebene.
No comments:
Post a Comment