EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU

Monday, March 17, 2014

ISEMAVYO MITANDAO: BLOGU YA FULL SHANGWE YASEMA: MKALI WA WIMBO NI `KWA NEEMA NA REHEMA`, EDSON MWASABWITE AKIRI KUPATA MAFANIKIO, NAKALA ZA KUTOSHA ZASAMBAZWA KILA KONA YA NCHI, AJIPANGA KUFYATUA ALBAMU MPYA!! - 2013

by John Bukuku on November 19, 2013

Bonyeza hapa kuona chanzo cha habari: FULL SHANGWE BLOGU

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam

MWIMBAJI anayechipukia kwenye muziki wa Injili , anayetamba na wimbo wa `Ni kwaneema na Rehema` Edson Mwasabwite amekiri kuwa wimbo huo umebadilisha maisha yake kuanzia kipato, kujulikana miongoni mwa watanzania wengi, ingawa hajafikia malengo yake.

Mwasabwite amesema hayo alipotembelea nyumbani kwa mhariri mkuu wa mtandao wa FULLSHANGWE, Baraka Mpenja na kuweka wazi kuwa mpaka sasa ameuza nakala za kutosha za wimbo wake uliomtoa katika tasnia ya muziki wa injili `Ni kwa Neema na Rehema`.

“Kwasasa hivi pesa niliyokuwa naitafuta kwa mwaka, ninaweza kuipata kwa siku moja. Hakika ni kwa neema kwani sikutegemea kama nitafika hapa nilipo ingawa najiona ndio kwanza naanza safari katika muziki wa injili”. Alisema Mwasabwite.

Mwasabwite ameongeza kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kama Mwenyezi Mungu angemshushia neema kama ilivyo sasa, kwani ametoka katika hali ya kushindwa kununua hata baiskeli na sasa anafikiria kupata usafiri wake wa kumsaidia kufanya kazi ya Mungu.

“Wimbo huu umenibadilisha maisha yangu, kwasasa mashabiki wengi wa muziki wa Injili wananihitaji kila sehemu ili nikafanye huduma. Kiukweli hata ratiba zangu zimebadilika, nimekuwa nikihitajika maeneo mengi sana kufanya matamasha, nami sichoki kwani nipo shambani mwa bwana”. Alisema Mwasabwite.

Katika mazungumzo yake, Mwasabwite amekiri kuwa kila jambo lina wakati wake, Mungu hutoa kwa wakati wake, ikifika wakati wako utapata na hutaamini muujiza utakaokutoea.

Mwimbaji huyo anayesikika kila kona ya Tanzania aliongeza kuwa kwasa anajiandaa kufyatua albamu mpya itakayobeba jina `Baba amenihurima asilimia Mia`.

“Nimeamua kuipa jina hili kwasababu mimi kama Mwasabwite sijafanya chochote zaidi ya Mungu kunihurumia na kunifikisha hapa nilipo kwa asalimia zote. Sikuwa na sababu, vigezo, na nilikuwa wa kushindwa na kuaibika, kufa, lakini mungu amenihurumia”. Alifafanua Mwasabwite.

Albamu hii inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa nyimbo za injili itakuwa na nyimbo 10 zenye ujumbe mkali wa kumsifu na kumtukuza Mungu.

Hata hivyo, Mwasabwite amelalamikia suala la watu wachache kuiba kazi za wasanii kwani huwa wanavuna wasipopanda, hivyo lazima mamlaka zinazohusika kulinda haki za wasanii sanjari na serikali kujikita zaidi kuwaokoa wasanii na majanga ya wizi huu.

Pia amewasihii mashabiki kuungana na wasanii kununua CD Halisi ili kujenga uchumi wa wasanii na nchi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment