EDSON MWASABWITE: NI KWA NEEMA TU
Friday, June 27, 2014
MFULULIZO WA MBEYA GOSPEL FESTIVAL: ANN ANNIE, RACHEL, MESS JACOB CHENGULA NA WAIMBAJI WENGINE WATIKISA MBEYA
Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kiliandaa tamasha linaloenda kwa
jina la Mbeya Gospel Festival likiwa na lengo la kuwataka wana Mbeya
kujiunga na chama hicho kwaajili ya kuwasaidia kujua haki zao za
kimuziki.
Katika tamasha hili kulikuwa na waimbaji wengi sana kama vile Mess Jacob Chengula, Ann Annie, Rachel Sharp, na wengine wengi. Watu walibarikiwa sana.
Katika tamasha hili kulikuwa na waimbaji wengi sana kama vile Mess Jacob Chengula, Ann Annie, Rachel Sharp, na wengine wengi. Watu walibarikiwa sana.
Kutoka kulia ni Rachel, Ann Annie
Rachel Sharp kutoka Sweden
Emmanuel Mabisa
Mess jacob Chengula mwenye koti jeupe
Ann Annie
Monday, June 23, 2014
MAZISHI YA MAREHEMU MCH> DEBORA SAID SIKU YA JUMATATU 23.06.2014
SIKU YA MWISHO YA KUMUAGA MAREHEMU DEBORA KATIKA KANISA LA MAISHA YA USHINDI UBUNGO EXTERNAL DSM SIKU YA JUMATATU 23.06.2014
Mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Debora Said amekuwa
dunia tangia mwaka 1972 na mwaka huu wa 2014 Juni Mungu amemchukua kwa
mapenzi mema. Mch.Debora Said amefanya kazi yake akiwa duniani,
amewaleta watu wengi kwa Yesu kwa njia ya uimbaji na uchungaji wake,
ameisaidia familia yake mbali na huduma yake ya uimbaji na uchungaji.
Katika
sherehe hii ya kumuaga Mch. Debora Said kulikuwa na waimbaji weng0i
sana, baadhi yao ni Upendo Nkone, Victor Aron, Joshua Makondeko,
Chidumule, Neema Gasper, Madam Ruti, Lungu la Yesu, Addo November,
Christina Matai, Miriam Lukindo, Chriss, Martha Mwaipaja, Kyambiki,
Petro, Apostle Gideon Mutalemwa, Upendo Kilahiro, na wengine wengi sana.
Askofu John Said mume wa marehemu Mch. Debora Said
Siku
hii ilikuwa ni siku ya furaha na shangwe kwa kumuaga mtumishi wa Mungu
Debora Said, waimbaji waliweza kuimba kwa furaha na bila kuonyesha
huzuni. Lakini haikuishia hapobali watu wengine walionekana wakitoa
machozi na kulia kwa sauti, na hii inaonysha ni jinsi gani Mchungaji
Debora Said alikuwa mchango mkubwa Tanzania na Afrika nzima.
Katika
sherehe hii kulihudhuriwa na wachungaji wengi sana kwaajili ya kumuaga
mpendwa wetu Mch. Debora Said. Wachungaji waliweza kutoa maneno machache
kukuhisiana na msiba huu na wengine walionekana wakishindwa kujikaza na
badala yake machozi yakiwatoka.
Rulea Sanga aliyekaa na shart nyeusi akitafakari
Tunamshukuru
sana Mungu kwa kumpa ujasiri mume wake na marehemu Askofu John Said,
alionekana ni mtu mwenye ujasiri kwa sura na akiwa na matumaini ya
kwamba mke wake ametwaliwa na Mungu wetu wa mbinguni. Kibinadamu
inaumiza sana kuona yule uliyekuwa unamtegemea kimawazo ametoweka
duniani. Hakika huu ni wakati mugumu sana kwa Askofu John Said na kanisa
lake zima kwa maana wameondokewa na mtu ambaye alikuwa kama nguzo ya
kanisa.
Kwa
wasiojua, ni kwamba marehemu Mchungaji Debora Saidi alikuwa ni
mwimbaji, Mchungaji na pia mwanamichezo (netball). Kutoakana na taarifa
tulizopata msibani ni kwamba alijituma sana katika ujuenzi wa kanisa lao
na pia alikuwa muhimizaji mkubwa katika swala zima la michezo.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Addo November aliwaomba waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania waache tabia ya kujiona mastaa na kujitenga na wengine wakati wa raha na shida. Alisema anayeweza kukuweka wewe kuonekana staa ni Yesu Kristo tu na sio mwanadamu, Mungu anaweza kukushusha na kumuinua mtu mwingine kwa kazi yake. Pia aliwataka wasijifananishe na watu wa Bongo Fleva kwani wao ustaa mara nyingi wanategemea votes za mashabiki na asilimia kubwa hawategemea kutoka kwa Yesu Kristo. Rais aliwashukuru waimbakji wote kwa usirikiano wao katika zoezi zima la kumuaga mtumishi wa Mungu Mch. Debora Saidi.
Mch mama Fednandes wa kanisa la AGAPE alitoa ofa ya kurusha matukio ya msiba huu wote katika kipindi cha FIRE katika television cha ATN na pia ameandaa tamasha kubwa la waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania hapo kanisani kwake.

KIPINDI CHA KUPELEKA MWILI WA MAREHEMU MCH. DEBORA SAID KANISANI
Wa pili kutoka kushoto ni Askofu John Said mume wa Marehemu Mch. Debora Said akijianda kuingia Kanisani
WAIMBAJI WAKISHREKEA SIKU YA PEKEE YA KUMUAGA MWIMBAJI MWEZAO MCH. DEBORA SAID
Tumaini Njole akimsindikiza rafiki yake Mch. Debora Saidi
Edson Mwasabwite akisema bye bye Debora Said huku akiimba wimbo wa Ni kwa Neema tu
MC Joshua Makondeko
Kwaya ya kanisa la Maisha ya Ushindi kwa Askofu John Said
Waimbaji kutoka Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) wakiimba wimbo maalum wa kumuaga mpendwa wao marehemu Debora Saidi
Edson Mwasabwite
Apostle Gideon Mutalemwa
Christina Matai hakuweza kujizuia, alijishtukia analia wakati waimbaji wenzake wakiimba. Hii inaonyesha ni jinsi gani alipigwa na kifo cha marehemu Mch. Debora Said
Sifa John
Kutoka kulia ni Victor Aron
Upendo Nkone
Lungu la Yesu
UKITAKA KUONA MATUKIO ZAIDI BOFYA HAPA: RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

Subscribe to:
Posts (Atom)