Baada
ya kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali, Grace na Joshu wameamua sasa
kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu.
Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu
kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada
yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati
umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya
albamu yao hii ya kwanza.
Grace Christian Rwegasha
Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni
alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa
hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa
nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja
kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema
katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya
Kiswahili ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi
na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo
za Kiingereza.
Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja
kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee
ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma
yao ya uimbaji.
Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la
muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha
St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi
anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba
katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko
Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.
Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi
ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao
katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya
kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba
ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao
kuwashirikisha
Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano
ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu
mbalimbali.
Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote
na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya
kazi ya Bwana.
Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa
wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya
utakaposikia mahojiano yetu.
Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080
MUNGU AKUBARIKI